Akihutubia baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian amewataka madiwani hao kuwachukulia hatua watendaji wote waliohusika kwenye matumizi mabaya ya fedha za Serikali. “Kwa kuwa baadhi ya hoja zilizotajwa na CAG zinatokana na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri kutowajibika ipasavyo au kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu, Wahusika wabainishwe na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria au za kinidhamu.” Alisema Dkt Batilda Burian.
Aidha amelitaka baraza hilo kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na kamati za Bunge ili kuhakikisha Halmashauri inatimiza wajibu wake. “bado kuna utekelezaji hafifu wa Maagizo ya kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC). Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ilipewa maagizo matatu (3), ambapo maagizo yote matatu (3) bado yanaendelea na utekelezaji”, alisema Dkt. Batilda Burian
Haya yamejili leo Juni 8, 2023 wakati Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian alipohudhuria Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Nzega cha kupokea taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyoishia Juni 30, 2022.
_________________
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa