Katibu Tawala (M) Tabora Dkt. John Mboya amewataka Wamachinga Mkoani Tabora kutoa ushirikiano wakati Serikali ngazi ya Mkoa ikiwekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa Ofisi ya Wamachina. Na kwamba Serikali ngazi ya Mkoa inatambua nafasi ya Wamachinga kwenye ukuaji wa Uchumi wa nchi.
Akiongea na Wamachinga leo kwenye Ukumbi wa The Citizen Hall, Dkt. John Mboya ameweka bayani nia ya Serikali ya kuwarasmisha Wamachinga kwenye taasisi ya kifedha ili kupata mikopo ya riba nafuu. Na kuwasisitiza kutumia mikopo hiyo kama inavyoelekezwa na sio kinyume chake.
Mapema leo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya aliwasili na kupokelewa na uongozi wa Shirikisho la Wamachinga (SHAUMA) kwenye Ukumbi wa The Citizen Hall kwa ajili ya kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwenye mkutano baina ya uongozi wa Serikali ngazi ya mkoa na baraza la SHIUMA Mkoa wa Tabora.
Malengo makuu ya mkutano huo ni ajenda , kanuni, taratibu na madodoso ya kuwatambua Wamachinga na kuona kwa namna gani Wamachinga wanaweza kufaidika na kutambulika rasmi katika taasisi za kifedha zikiwemo Benki ili kuweza kufaidika na fursa na huduma zingine.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa