NA TIGANYA VINCENT
MAAFISA Utumishi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora wametakiwa kutatua kero zinazowakabili watumishi katika maeneo ya kazi ili kuweka mazingira ya wao kutoa huduma bora kwa wananchi
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kutoka Halmashauri za Mkoa huo.
“Kama mnavyoshughulikia maslahi yenu kwa bidii …fanyeni hivyo hivyo kwa watumishi waliochini yenu ili kuondoa manuniko” amesema.
Amesema ni vema wakafanyia kazi manunuko na matatizo yanayowakabili watumishi katika Halmashauri zao ili wawe na moyo wa kufanyakazi na kuleta matokeo mazuri katika jamii.
Makungu amesema Maafisa Utumishi wanalojukumu la kuhakikisha watumishi wanapata stahili zao kwa mujibu Sheria na Taratibu.
Ametaja stahili hizo ni pamoja na kumlipa mtumishi posho apohamishwa na kumlipa fedha za nauli ya mkurudisha kwao mtumishi anapostafu kazi.
Makungu amesema kushindwa kulipa stahili za watumishi kwa wakati kunaweza kusababisha Serikali kupelekwa Mahakamani kwa sababu ya Afisa Utumishi kushindwa kutekeleza jukumu lake ipasavyo.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa ameonya Watumishi kuhamishwa bila kufuata taratibu na wakati mwingine kutoa uhamisho wa kumukomoa mtumishi.
Aidha Makungu amewataka Maafisa Utumishi kuwa na ratiba ya Watumishi wote wanaokaribia kustaafu ili waweze kuwaandalia mapema stahiki zao.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa