Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya amewahakikishia viongozi wa dini mkoani Tabora na Tanzania kwa ujumla kuwa Serikali inatambua mchango wa viongozi wa dini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ustawi wa jamii yetu.
Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika sherehe za Baraza La EID AL ADHa iliyofanyika June 29, 2023, Dkt. John Mboya amefafanua kuwa “Kutokana na changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu, Serikali kwa Kushirikiana na Taasisi mbalimbali imekuwa ikishirikiana katika kuhakikisha kwamba vizazi vyetu vinakuwa na maadili mema yanayompendeza Mungu.
Aidha katika kuhakikisha Serikali inatekeleza mipango yake ya maendeleo Dkt. John Mboya ameeleza kuwa “tuendelee kuunga mkono Mkoa wetu chini ya ongozi shupavu wa Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian, akimwakilisha Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kutoa huduma bora za kijami”
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa