• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC ATOA SIKU SABA KWA FAMILIA 10 AMBAZO ZIKO ENEO LA BONDE LA WEMBERE WILAYANI IGUNGA KUONDOKA

Posted on: April 20th, 2021

RC ATOA SIKU SABA KWA FAMILIA 10  AMBAZO ZIKO ENEO LA BONDE LA WEMBERE WILAYANI IGUNGA KUONDOKA

 FAMILIA kumi za wafugaji na wakulima ambazo bado zilikuwa zimebaki katika eneo la  Bonde la Wembere lilipo wilayani Igunga licha ya wenzao kutii maagizo ya Serikali zimepewa siku 7 kuondoka hiari kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Agizo hilo limetolewa  na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati alipofanya ziara katika eneo la Bonde la Wembere kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa agizo la kuwtaka watu waliokuwa ndani ya bonde hilo kuondoka kwa hiari.

Alisema hadi hivi sasa zaidi ya familia 200 zimeondoa kwa hiari katika eneo hilo na kwenda katika eneo maalumu ambalo wapengangiwa na Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na Wilaya lakini hizo familia 10 zimeendelea kubaki licha elimu waliyopatiwa katika mkutano wa hadhara.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema katika mkutano na watu hao ulifanyika katika kijiji cha  Makomero mapema mwezi uliopita walikubaliana kaya 13 kati ya 200 ambazo zilikuwa bado ndani bonde hilo ziondoke na ziende eneo walilopangiwa ,lakini ni kaya tatu ndio zilitekeleza agizo hilo na kaya 10 zimendelea kubaki.

Alisema kususua kw familia hizo kuondoka kunasababishwa na baadhi yao kuwapotosha kuwa wasiondoke .

Kufuatia hali hiyo, Dkt. Sengati alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo kwa kushirikiana na Polisi wa Igunga kumtafuta kinara wa mgomo huo ambaye ni Kiongozi wa kundi la Wakulima Kilimanjalo Masandu Masaganya na wenzake wawili ambao wamekuwa wakiwahamasisha wenzao kutoondoka ili kujua nani yuko nyuma yao.

“Hizi kaya 10 zilizobaki ndani za siku 7 ziondoke ili Serikali iweze kutekeleza majukumu yake katika eneo hili …ndani za siku saba sitarajii kuzikuta kaya hizi zikiwa bado ndani yake”alisisitiza.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hatarajii kuona wanasiasa wanatumia siasa katika eneo hilo ambalo lina maslahi mapana kwa  maendeleo ya nchi na kuongeza kuwa Tanzania sio kisiwa imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ya kutunza na kuhifadhi maeneo oevu.

Alisema ni kinyume cha Sheria kaya hizo kuendelea kuwemo humo, kwa kuwa eneo hilo ni mali ya Serikali na linayo maslahi mapana ya nchi ikiwemo utafiti wa gesi na mafuta unaondelea na eneo hilo ni chujio la maji kuelekea Ziwa Eyasi.

Dkt. Sengati alitaja  maslahi mengine  yanayopatikana humo ni pamoja na uwepo wa aina ya Flamingo ambao wanapatikana maeneo machache duniani na bonde hilo ni njia ya wanyamapori kuelekea Pori la akiba la Rungwa.

Kufuatia Mkuu huyo wa Mkoa alisema ofisi yake itafanya majadiliano na  Ofisi ya Makamu Rais Mazingira, Wizara ya Maliasili na Utalii , Wizara ya Nishati , Wizara ya Maji na Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi ili waweze kuanisha eneo ambalo lina maslahi mapana ya nchi na litakalobaki wapewe wananchi kwa utaratibu mzuri.

Alisema kaya zilizobaki katika eneo hilo zimejimilikisha maeneo makubwa ambayo ni mali ya Serikali na kuyatumia kwa maslahi binafsi ya kuwakodisha wafugaji kutoka maeneo mbalimbali kulisha mifugo yao na kuendelea kusababisha uharibifu katika bonde hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema wataendelea kuhakikisha maeneo yote ya hifadhi yanalindwa na kuzuia wavamizi kuingia kwa ajili ya kuendesha uharibifu ndani yake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga (OCD), Ally Mkalipa alisema Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Igunga ilikwenda katika eneo hilo ili kutathimini kaya zilizomo ndani yake  na kukaa nao kikao wakakubali na kuonyeshwa eneo watakalohamia ambao walilipenda na kaya nyingi zilihamia na kuondoka katika bonde hilo , lakini kuna kaya ambazo zimekataa kuhamia katika sehemu walizopangiwa.

Alisema kitendo cha familia 10 kuendeleaa kubaki ni ukaidi na kukiuka makubaliano na hivyo watachukua hatua kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Nchi.

Mkalipa alisema familia hizo ni wakaidi kwa kuwa watumia mbinu za wanaume kujificha nyakati za mchana na kuacha watoto  na wanawake na ikifika usiku ndipo wanarudi na baadhi yao wanadiriki hata kuwahamasisha wenzao wasiondoke kwenda walipopangiwa na Serikali ya Kijiji kwa kushirikiana na Wilaya.

 

mwisho

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa