RC AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUSIMAMIA VEMA UKUSANYAJI WA MAPATO
MAMLAKA za Maji na Jumuiya za Watumiaji Maji(COWSO) Mkoani Tabora zimetakiwa kuhakikisha zinasimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na uuzaji maji ili miradi hiyo iwe endelevu.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Philemon Sengati wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kutoka maji ziwa Victoria kwenda Mkoani humo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema miradi yote inayotokana na uwepo mradi wa maji ya ziwa Victoria ni lazima iendelee kuhakikisha mitando ya maji ya bomba inasambazwa kwa wananchi ambao wako katika eneo la mradi nab ado hajawafikiwa na huduma hiyo.
“Lazima muendelee kupanua zaidi mtandao wa maji kwa kujenga mitandao ya bomba , matanki mengi na kuweka magati mengi ili wananchi waweze kuendelea kufaidi matunda ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuondolea adha ya upatikanaji wa maji” alisema
Dkt. Sengati aliongeza Mamlaka za Maji kwa kushirikiana na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) zinatakiwa kuendelea kuzijengea uwezo Jumuiya za watumiaji maji ili ziwe kutoa huduma nzuri kwa wananchi wengi.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoani Tabora kuwa na mpango wa wateja wenye kipato cha chini kulipa kwa awamu gharama za kuunganishiwa mtandao wa maji ili nao waweze kunufaika na huduma ya maji kutoka ziwa Victoria.
Alisema hatua hiyo itatimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ya kutaka watu wengi wapate huduma ya majisafi na salama karibu na wanapoishi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora Dkt. Sengati amezitaka Mamlaka hizo kuwa na utamaduni wa kuagiza vifaa kwa wingi vya kuunganisha mtandao wa maji moja kwa moja kutoka viwandani.
Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za kuwaunganishia maji wananchi wanazotozwa wakati wanapoomba huduma hiyo.
Dkt.Sengati alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha maji yanawafikia wananchi wengi popote walipo ili wawaze kushiriki katika shughuli za maendeleo.
“Wananchi wakipata majisafi na salama watakuwa na afya bora ambayo itawaweza kutumia muda ambao walikuwa wakiutumia kutafuta maji na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo” alisisitiza.
Alisema kitendo cha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wingi kaika maeneo yao kitachochea ukuaji wa uchumi na kuwawezesha kuwekeza katika shughuli mbalimbali na kuwavutia wawekezaji kutoka nje.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora anaendelea na ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa