Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, amefika na kujionea shughuli mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete, iliyopo Manispaa ya Tabora, Mkoani Tabora, Novemba 11, 2023.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alitembelea jengo la wagonjwa wa Dharura( EDM), jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), jengo la mionzi na jengo la mama na mtoto.
Ambapo jengo la wagonjwa wa Dharura( IDM), jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) na jengo la mionzi yameshakamilika na yameanza kutoa huduma wakati huo huo jengo la mama na mtoto ujenzi wake bado unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiongea na baadhi ya wananchi waliofika Hospitali ya Kitete kwa ajili ya kupata Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete, Novemba, 11, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipata maelezo kutoka kwa Afisa Muuguzi Ndugu. Rose Mkata kwenye kitengo cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) kulichopo Hospitali ya Rufaa ya Kitete, alipotembelea katika hospitali hiyo Novemba 11, 2023.
Afisa Muuguzi Hospitali ya Rufaa Kitete, Ndugu. Rose Mkata Ameeleza kuwa hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa sana kuhudumia wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura na huduma ya wagonjwa wanaohitaji uangalifu Maalumu ambapo amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa fedha ambazo zimetumika kununua vifaa tiba vyote na tayari huduma imeshaanza kutolewa hospitalini hapo.
Na mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Muuguzi, Mkuu wa Mkoa amewaagiza watendaji wa hospitali hiyo kuhakikisha miundombinu yote inayohitajika inakuwepo kwenye majengo yote ya Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na Dharura ili kuhakikisha wananchi wanaofika hospitalini hapo wanapata huduma bora na za kisasa zaidi.
Aidha ameongeza kuwa, majengo haya yanafanya kazi kwa kutegemeana, kwamba Wagonjwa watapokelewa katika jengo la dharura na kisha kupelekwa kwenye jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipata maelezo baada ya kuingia na kukagua kwenye jengo jipya la mionzi lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Na mpaka sasa jengo limekamilika na vifaa vyake vyote na tangu kuanza kwake jengo la mionzi limeshahudumia wagonjwa zaidi ya Arobaini (40).
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipata maelezo kutoka kwa Makandarasi wa Kamapuni ya Ujenzi ya Masasi Construction Co Ltd Ndugu. Joseph Masonga baada ya kutembelea na kukagua jengo la mama na mtoto ambalo linaendelea na shughuli za ujenzi.
Mpaka sasa ujenzi umefikia katika hatua ya pili ambapo jumla ya fedha shilingi Bilioni 5.198 zimetumika katika ujenzi huo.
Baada ya kupata maelezo na kutembelea jengo hilo Mkuu wa Mkoa ametoa siku 3 kwa mkandarasi huyo kumaliza baadhi ya kazi ambazo zilipaswa kukamilishwa katika hatua ya kwanza ya ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi katika kitengo cha Watoto Elinasoe Nacha kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete, alipofika hospitaliani hapo Novemba 11, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa