Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amepokea na kukabidhi msaada wa nguo aina ya “truck suit” na madaftari aina ya “counter book” ikiwa ni muendelezo wa msaada kutoka Benki ya NMB Kanda ya Magharibi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ziba ambao mnamo Januaro 23, 2024 uliunguliwa na vitu vyo kufuatia ajali ya moto iliyosabisha kuungua kwa bweni la wavulana shuleni hapo.
Akipokea masaada huo, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ambao kwa hakika umekuwa na tija kwa wanafunzi hao ambao licha ya jambo hili limetokea ghafla, benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele wa kuhakikisha Watoto wanafunzi hawa wanapatiwa msaada wa haraka.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Ndugu. Seka Urio amesema kuwa Benki ya NMB imetoa msaada huo wenye thamani Zaidi ya shilingi milioni saba (7) kwa wanafunzi hao ikiwa ni moja ya juhudi za benki hiyo katika kurudisha faida zake kwa jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii. Na kwa kipindi chote benki ya NMB itaendelea kuunga mkono serikali katika kusaidia jamii.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa