Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia maafisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania na wananchi waliojitokeza kwenye ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Akitoa Hotuba yake, Mhe. BalozI Dkt. Batilda Salha Burian ametoa wito kwa wananchi wa Tabora kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi La Wananchi Tanzania ili kuhakikisha uhalifu unapungua na suala la usalama linakuwa ni la kila mmoja wetu.
“Kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora natoa wito kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania katika kukabiliana na uhalifu. Jukumu la usalama wa Nchi si la vyombo vya ulinzi na usalama tu bali ni kwa kila mwananchi.”
Sambamba na hilo Mhe. Batilda amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amir Jeshi Mkuu, kwa kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kuwepo kwa kuwa na vymbo imara vya ulinzi ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana na kwa kushirikiana.
“Nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha vyombo vya ulinzi vinafanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha amani na usalama unapatikana kwa wakati wote na kutoa nafasi kwa wananchi kujionea kazi Kubwa inayofanywa na Rais wetu na jana tu tuliweza kupokea magari sita na mawili yakiwemo ya Jeshi la Polisi”
Aidha Mkuu Wa Mkoa ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu waache mara moja kwani vyombo vya ulinzi vipo imara kila wakati na yeyote atakaye jaribu kuchezea amani iliyopo atashughulikiwa ipasavyo na Vyombo vyetu.
“Kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora natoa wito kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana na uhalifu. Jukumu la usalama wa Nchi si la vyombo vya ulinzi na usalama tu bali ni kwa kila mwananchi.”
Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian iliyoitoa wakati wa ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Alli Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiimba wimbo wa uhamisishaji kwa maafisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania walioshiriki kwenye ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwahamasisha baadhi ya wananchi kuimba wimbo wa uzalendo, waliojitokeza kwenye zoezi zima la ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu sambamba na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Jeshi la Wananchi Tanzania na baadhi ya watoto waliojitokeza kwenye ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Aly Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu sambamba na kamati ya Usalama ya Mkoa wa Tabora, na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania mara baada ya ufungaji wa Zoezi la “Taifa Salama” uliofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Zoezi la “Taifa Salama” ni zoezi ambalo limeendeshwa kuanzia tarehe 12 Novemba 2023 hadi leo hii tarehe 17 Novemba 2023, limehitimishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Manispaa ya Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa