Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametembelea na kujionea kiwanda kidogo cha kuchakata mazao ya nyuki kilichopo kata ya Nkiniziwa, wilayani Nzega na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika kiwanda hiko kinachosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Mhe. Mkuu wa mkoa ametoa wito kwa viongozi wa TFS kuhakikisha wanatilia mkazo shughuli za uzalishaji wa asali ili kuhakikisha kiwanda hiko hakikosi malighafi, sambamba na kufuata hatua stahiki za uchakataji ili kulinda ubora wa asali.
Dkt. Batilda amewataka viongozi wa wilaya ya Nzega kuhakikisha wanashirikiana na wadau katika kutoa elimu ya uzalishaji wa asali ili kuhakikisha kiwanda hiki kinakuwa na tija kwa wananchi wilayani humo na Tabora kwa ujumla.
Akisoma taarifa ya mradi, Msaidizi wa ufugaji nyuki TFS, KamandaLoveness Malle amesema kuwa, utekelezaji wa mradi huo uliogharimu shilingi milioni 111.3 (Fedha kutoka mfuko wa Misitu Tanzania) umekamilika kwa asilimia 99 na tayari mitambo imeshawekwa kwa ajili ya kuanza shughuli za uzalishaji.
Naye, Mwakilishi kutoka Makao Mkuu (TFS) kanda ya Magharibi, Muhifadhi Mkuu mkoa wa Tabora Aloyce Kilemwa amemuhakikishia Muheshimiwa mkuu wa mkoa kutekeleza maagizo yote yaliotolewa ili kuhakikisha kiwanda hiko kinafanya kazi kwa malengo yaliokusudiwa.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Katibu Tawala Bi. Winfrida Funto ameweka bayana mikakati ya serikali katika utunzaji wa mazingira na tayari wilaya imeshasambaza miti zaidi ya milioni 3.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa