• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC CHACHA AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKETEZA SHAMBA LA BANGI KATIKA ENEO LA HIFADHI YA NYAHUA MBUGA SIKONGE.

Posted on: June 6th, 2025


Na. OMM Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Paulo Chacha, ameongoza oparesheni maalum ya kuteketeza shamba kubwa la bangi lililolimwa  ndani ya Msitu wa Hifadhi wa Nyahua Mbuga, wilayani Sikonge. Shamba hilo linakadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari 3 na eneo la hifadhi hiyo lina ukubwa wa  hekta 679,000, hatua ambayo imeibua taharuki na mshangao kutokana na kiwango kikubwa cha uvunjifu wa sheria.

Oparesheni hiyo ilihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora, Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Sikonge pamoja na watendaji wa serikali kutoka ngazi ya mkoa na wilaya. Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia taarifa za kiintelijensia zilizowasilishwa na vyombo vya usalama kuhusu uwepo wa kilimo haramu katika eneo la hifadhi.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo, Mhe. Chacha alionesha masikitiko makubwa juu ya kitendo cha baadhi ya wananchi kuamua kwa makusudi kuingia maeneo ya hifadhi kinyume na sheria, kisha kuendesha shughuli haramu za kilimo cha bangi.

“Haiwezekani tukavumilia uhalifu wa waziwazi kama huu. Sheria lazima ifuate mkondo wake. Tunatoa onyo kali kwa wote wanaojihusisha na kilimo hiki haramu, wasitafute kuhalalisha uovu katika maeneo ya hifadhi,” alisisitiza Mhe. Chacha.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Tabora na maeneo jirani kuacha mara moja tabia ya kuingia katika maeneo ya hifadhi kwa shughuli yoyote ile bila kibali, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, alisema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini watu wote waliohusika katika kilimo hicho haramu.

Tukio hili linakuja wakati ambapo juhudi za serikali za kupambana na uhalifu wa mazingira na dawa za kulevya zimeongezwa, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kulinda rasilimali na kuhakikisha ustawi wa wananchi.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RC CHACHA AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKETEZA SHAMBA LA BANGI KATIKA ENEO LA HIFADHI YA NYAHUA MBUGA SIKONGE.

    June 06, 2025
  • MHE. CHACHA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI WILAYANI URAMBO: KWA KUFANYA USAFI, KUPANDA MITI NA KUTOA WITO WA KUTUNZA MAZINGIRA.

    June 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI - JUNI 5, 2025.

    June 04, 2025
  • SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 26.9 KUWAINUA WAKULIMA KUPITIA MRADI WA UMWAGILIAJI MWAMAPULI – IGUNGA

    June 03, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa