MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuharakisha ujenzi wa machjio ya kisasa kwa ajili ya kuongeza chanzo cha mapato,
Alisema hali itasaidia uboreshaji wa nyama inayozalishwa kila siku,
Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo leo mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora.
Alisema Nchi nyingi zikiwemo za Kiarabu zinahitaji nyama kwa wingi kutoka Tabora bali kinachotakiwa ni kuwa na machinjio ya kisasa ambayo itasaidia kuongeza thamani yake.
Balozi Dkt. Batilda aliwataka wafanyabishara kama wabia wa Serikali katika masuala ya maendeleo kushirikiana na Manispaa ya Tabora katika kuboresha sekta ya nyama ili waweze kujiongezea kipato.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema Serikali itajitahidi kuwatafutia kibali kitakachowawezesha kusafisha nyama nje ya Nchi bila matatizo,
Balozi Dkt. Batilda alisema katika kuhakikisha kuwa watakapokuwa tayari kusafisha nyama hadi nje ya Nchi wameliomba Shirika la Reli Tanzania kuandaa Mabehewa ambayo yanaweza kusafisha nyama bila kuharibika,
Aliongeza sanjari hilo Nchi za Kiarabu zinahitaji sana asali na kuwataka kutumia mizinga ya kisasa katika uzalishaji na kuiongezea thamani ili iweze kuwa na soko kubwa duniani,
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa