• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AAGIZA UPANDAJI WA MITI YA MATUNDA MASHULENI

Posted on: October 24th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza kila shule ihakikishe imepanda miti ya matunda katika maeneo yao.

Hatua hiyo inalenga kuongeza wingi wa matumizi ya matunda kwa ajili ya wanafunzi wawapo shuleni na kukamilisha mzunguko wa lishe bora.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya lishe ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Tabora chini ya kauli mbiu Lishe bora ni kinga thabiti ya magonjwa kula mlo kamili fanya mazoezi kwa bidii  kazi iendelee.

Balozi Dkt. Batilda alisema hata kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza ulaji wa mlo kamili hauwezi kukamilika bila kuwepo kwa tunda katika chakula.

Aliwataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote Mkoani kuhakikisha wanawahimiza wananchi wakiwemo wanafunzi kupanda miti ya matunda ya aina mbalimbali katika maeneo yao.

Balozi Dkt. Batilda alisema hatua hiyo itaongeza upatikanaji wa matunda kwa ajili ya wao kula na yale ya ziada watauza na kujiatia fedha kwa ajili shughuli zao za maendeleo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Watendaji katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI Tumbi) kuhakikisha inasambaza teknolojia ya upandaji wa miti ya matunda na ile ya dawa asili ili isitoweke.

Alisema baadhi ya matunda pori yanafaida nyingi mwili ikiwemo kutumika kama tiba na kinga mwilini.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilda aliwataka wakazi wa Tabora na wageni waliopo katika maadhimisho hayo kutembelea eneo maalumu la mapishi ya vyakula vya asili  kwa ajili ya kujifunza mapishi mbalimbali.

Alisema vyakula hivyo ni muhimu kwa kulinda afya kwa kuwa vinatumia viungo vya asili kama vile karanga na havitumii mafuta mengi.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilele cha maadhimisho ya wiki ya lishe kitafanyika Jumamosi ya wiki hii ambao Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Afya  Maendeleo ya Jamii  Jinsia  Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda alisema kwa kuwa Mwezi ujao wanaanza zoezi la kutoa chakula mashuleni atakwenda usimamia zoezi la upandaji wa matunda  ili wanafunzi wanaokula chakula mchana wapate na matunda kwa ajili ya kukamilisha mlo kamili.

Wakati huo huo Wakuu wa Wilaya wamesaini Mkataba wa utekelezaji wa masuala ya lishe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili waweze kusimamia vizuri masuala ya lishe.

Akizungumza baada ya kuwasainisha mikataba hiyo , Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda aliwataka kuhakikisha masuala ya kuhamasisha  lishe ni ajenda ya kudumu.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitambua umuhimu lishe na ndio maana akasisi na kusisitiza masuala ya lishe hapa nchini wakati akiwa Makamu wa Rais.

Balozi Dkt. Batilda alisema Rais Samia alitambua kuwa kupitia lishe bora Watoto wanaozaliwa wanakuwa na king ana afya bora

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE. CHACHA AIPONGEZA TIMU YA UMISSETA MKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA

    July 01, 2025
  • RC. CHA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA, WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU.

    July 01, 2025
  • TABORA: MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA MAADILI YA NCHI

    June 26, 2025
  • MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA YAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA MATUMIZI YA MFUMO WA PEPMIS KWA WATUMISHI WA UMMA MKOA WA TABORA

    June 23, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa