Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili Wilayani Uyui Kuhudhuria Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Katika mkutano Huo Mkuu wa Mkoa alikabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari ya Itede na Ndono na kisha kuhutubia baraza hilo la Madiwani.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM (W) Uyui Ndugu. Said Makoba akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi CCM katika Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mhe. Said Ntahondi akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Novemba 10,2023
Katika sehemu kubwa ya taarifa yake ametoa pongezi na kumshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya ziara Mkoa Tabora ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa Wilaya ya Uyui na Tabora kwa ujumla.
Pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwa kusimamia vema miradi ya maendeleo Mkoani Tabora, na kujitoa katika kipindi chote cha Ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Na mwisho amempongeza kwa kusimamia suala la michezo hususani Timu ya Tabora United ambayo inaendelea kufanya vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikabidhi zawadi kwa Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya Kidato cha Sita Mwaka 2023 kutoka Shule ya Sekondari Idete na Ndono katika Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia balaza la madiwani katika Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Katika sehemu kubwa ya hotuba yake, Mhe. Mkuu wa Mkoa amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedhi nyingi kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeeo ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo. Ambapo miradi yote hiyo Mkoa wa Tabora unaendelea kufaidika kwa kiasi kikubwa sana.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwa watendaji wote wa Wilaya ya Uyui kusimamia fedha zinazolusanywa na zile ambazo zinatumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Amesisitiza uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa Umma.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akitoa neno la Shukrani mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kuhutubia katika Kikao cha Balaza la Madiwani, Mkutano wa Kwanza wa Mwaka 2023/2024 unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Akitoa neno la shukrani Mhe. Zakaria Mwansasu amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kusimamia na kutekeleza maelekezo yate ambayo ameyatoa wakati wa hotuba yake.
Aidha, Mhe. Zakaria ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi ambazo Wilaya ya Uyui inazitumia kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Eimu na Afya.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa