Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametembelea na kufanya ukaguzi kwenye mradi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa (Tabora Girls Grand) iliyopo kata ya Igagala, wilayani Kaliua, na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa mpaka sasa.
Mhe. Batilda Burian amewaagiza wasimamizi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopagwa na kwa viwango vinavyotakiwa, na kusitokee sababu za kutokukamilisha mradi huo mkubwa ambao Serikali imetoa fedha nyingi sana.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amemshukuru na kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha ambazo zinakwenda kukamilisha mradi huu mkubwa na wenye faida kwa wanatabora na watanzania kwa ujumla. Na kuahidi kuusimamia mradi huo mpaka utakapokamilika ili kurinda thamani ya fedha zilizotolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt Rashid Chuachua amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, kusimamia na kutekeleza maagizo yote yaliotolewa ili maradi huo ukamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa. Hadi sasa tayari kumeshafanyika jitihada mbalimbali za kuleta umeme ili shughuli za ujenzi zifanyike usiku na mchana.
Ujenzi huo mpaka sasa umegharimu shilingi Bilioni 3 ambazo tayari Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imeshazipokea. Na unatarajiwa kukamilika mnamo Disemba 30, 2023 na kuchukua wanafunzi 1280 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa