“Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mwaka 2021, Mkoa ulikuwa na hati chafu mbili(2), lakini kwa mwaka huu mkoa hauna hati chafu kutokana na Mkoa kuwa na uongozi imara na wenye kusimamia kikamilifu fedha za serikali” Alisema Dkt. Batilda Salha Burian.
Asisitiza malipo na makusanyo yote yanayohusu fedha za serikali yapitie kwenye mfumo rasmi wa serikali ili kuhakikisha mapato na matumizi ya serikali yanasimamiwa kikamilifu. Na pia kila halmashauri kutenga fedha 10% kwa ajili ya mikopo ya wanawake na wenye uremavu. Na kuzingatia suala la uwajibikaji unaofuata sheria.
Amelitaka baraza kuchukua hatua kwa mtumishi yeyote aliyehusika kwenye uzembe wowote wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali. “Kama wakaguzi wa ndani wapo kwanini tupate hati chafu?” Alisema Dkt. Batilda Salha Burian.
Aidha Dkt. Salha Burian amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake imara ambao kwa miaka miwili mkoa wa Tabora umefanikiwa kwenye sekta zote, na kuahidi kusimamia miradi yote inayotolewa na serikali.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa