Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian leo Julai 11, 2023 amekutana na wadau wa michezo Mkoani Tabora kwenye Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi kwa lengo la kujadiliana mambo yanayohusu sekta ya Michezo hususani suala la maandalizi ya Uwanja wa Al- Hassan Mwinyi unaotarajiwa kutumika katika michuano ya ligi Kuu Daraja la Kwanza.
Akizungumza na wadau , Mkuu Mkoa Dkt. Batilda amewapongeza wadau hao kwa kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha Mkoa wa Tabora unashiriki kwenye ligi kuu daraja la kwanza kwa mwaka 2023/2024 kupitia timu ya TABORA UNITED.
“Kama Mkoa tunawapongeza sana kwa kujitoa kwenu kwenye sekta ya michezo hususani mpira wa miguu na kufanikisha timu ya KITAYOSCE na sasa ni TABORA UNITED kushiriki kwenye ligi kuu daraja la kwanza na kwamba Mkoa wa Tabora umebarikiwa kuwa na wadau wenye mapenzi na timu zao za nyumbani”
Kuelekea kwenye ukarabati wa uwanja wa Al-Hassan Mwinyi, Dkt Batilda amewaomba wadau hao kutafuta namna ya kuhakikisha wanajitoa ili kuhakikisha uwanja huo unakidhi vigezo vinavyotakiwa kwa kuwa na huduma zote muhimu zinazohitajika.
“Niwaombe ninyi wadau wa michezo, kuangalia kwa namna gani tunaweza kufanya maboresho kwenye uwanja wetu ili uwanja huo uweze kutumika kwenye ligi kuu daraja la kwanza, kwani Mkoa wa Tabora umepata bahati kubwa kupata timu ambayo itashiriki ligi Kuu Daraja la Kwanza, kwetu ni fursa kubwa sana na sisi kama viongozi wa Mkoa tunatambua mchango wenu kwenye maendeleo ya michezo”
Kwa kutumia Kauli Mbiu ya “TABORA BILA LIGI KUU HAIWEZEKANI” Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Salha Burian aliwaongoza Wanatabora na kufanikisha timu ya KITAYOSCE na sasa TABORA UNITED kufuzu na kuingia Ligi Kuu Daraja la Kwanza mnamo Mei 13, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa