Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akisalimiana na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya Kardinali Rugambwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege Mkoani Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkaribisha Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya kumpokea alivyowasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa pamoja na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki na Serikali Pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa Mapokezi ya Kardinali Rugambwa katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili kwenye Kanisa la Katoliki Jimbo Kuu Katoliki la Tabora kwenye Ibada Maalumu ya Mapokezi ya Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya Kardinali Rugambwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege Mkoani Tabora
Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amesema Serikali inatambua mchango wa Kanisa Katoliki katika maendeleo ya Sekta ya Elimu na Afya. Na hivyo Serikali itaendelea na kufanya kazi na kushirikiana vema na Kanisa Katoliki pamoja na madhehebu mengine ya dini hapa nchini. Amempongeza Kardinali Rugambwa kwa kuendelea kuhubiri amani na umoja wa Watanzania na kumsihi kuendelea kuwa chachu ya amani, upendo na umoja.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameeleza kuwa, ni baraka kwa taifa na mkoa wa Tabbora kwa kupata Kardinali, na ndio maana hata wakati wa mapokezi manyunyu ya mvua yalinyesha n ahata kwa upande wa timu yetu ya Tabora United inazidi kufanya vizuri. Kwa hakika hizi ni baraka ambazo zinazidi kumiminika.
Akitoa salamu za shukrani Mwadhama Kardinali Rugambwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kanisa, Serikali na watanzania wote waliojitokeza kwenye mapokezi haya tangu anafika nchini na leo amefik hapa Mkoani Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa