Kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amefika Ofisi za Jimbo Kuu la Katoliki Tabora na kutoa salamu za pongezi kwa Baba Askofu Mkuu Protase Rugambwa kwa kuteuliwa na Baba Mtakatifu Fransisco kuwa Kadinali.
Tarehe 13 Aprili 2023, Baba Mtakatifu Frascisco alimteua Askofu Mkuu Protase Rugambwa kuwa Askofu Mkuu wenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania. Na mnamo June 25, 2023 Askofu Mkuu Protase Rugambwa alipokelewa na kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Tabora. Askofu Rugambwa na Maaskofu wengine 17 kutoka mataifa mbalimbali watasimikwa rasmi Septemba 30, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa