• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AMWAGIZA RAS KUPELEKA WAUGUZI KATIKA ZAHANATI YA CHAMPERA WILAYANI IGUNGA

Posted on: July 25th, 2019

RC TABORA AMWAGIZA RAS KUPELEKA WAUGUZI KATIKA ZAHANATI YA CHAMPERA WILAYANI IGUNGA

  

KATIBU Tawala Mkoa (RAS) Mkoani Tabora ameagizwa kuhakikisha anapeleka watumishi wa sekta ya afya katika Zahanati Chapera wilayani Igunga ili ianze mara moja kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa eneo hilo.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri  wilayani Igunga wakati wa  Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili hoja mbalimbali za Mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.

Alisema wakati Mkoa ukisubiri ajira za watumishi wapya ni vema Katibu Tawala Mkoa kuangalia uwezekano wa kuwagawanya watumishi waliopo kazi katika Zahanati ya Champera na maeneo ambayo hayana watumishi ili wananchi wa maeneo hayo nao waweze kupata huduma za afya karibu na mazingira yao.

 Mwanri alisema hoja ya Mkaguzi wa Nje ni vema ikatatuliwa kwa kugawanya watumishi waliopo katika vingine katika maeneo yasiyokuwa na watumishi kabisa.

 Katika hatua nyingine Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imeagizwa kuhakikisha inakusanya deni la shilingi milioni 42.4 kutoka kwa wananchi ambao hajawalipia viwanja walivyouziwa.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alitoa hoja hiyo na kuungwa mkono la Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kufuatia hoja ya Kamati ya Ukaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Nje baada ya kubaini deni hilo.

 Alisema kiasi cha deni hilo ni lazima kikuswanywe na hatua zichukuliwe ikiwa ni pamoja na wahusika kupewa mwezi mmoja ili walipe madeni yao na wakishindwa viwanja hivyo virejeshwe katika Halmashauri.

 Mwanri alisema baada ya Mwezi mmoja kuisha wahusika ambao wameshindwa kulipia vijanywa wanyang’anywe na viuzwe kwa wengine ili kulipa deni hilo.

 Kwa upande wa Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mku wa Hesabu za serikali (CAG) Erasto Juma alisema jumla ya mapato ya shilingi milioni 42.4 yaliyotokana na mauzo ya viwanja kwa wanunuzi 76 katika maeneo ya Nkokoto hayakuweza  kukusanywa.

 Alisema ni kiasi cha milioni 4 tu ndizo zilizokusanywa na kusalia kwa deni hilo.

 Halmashauri ya wilaya ya Igunga katika ukaguzi wa Hesabu unaoishia Juni 30 imepata hati inayoridhisha.

 

MWISHO.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa