Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, viongozi wengine wa Wilaya, kwa kushirikiana na Watumishi pamoja na Wananchi wa Tabora wameupokea Mwenge wa Uhuru, leo Septemba 14, 2023.
Awali, akiupokea Mwenge wa Uhuru, mapokezi yaliyofanyika katika Kata ya Kiloli Wilayani Sikonge, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Balozi Dkt Batilda amesema Mkoa wa Tabora upo tayari kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote nane (8) na utazindua miradi ya maendeleo Hamsini (50) yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2. Mkoa wa Tabora umeupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mbeya..
Salamu za Awali za Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2023
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, Ndugu. Abdallah Shaibu Kaim, ameweza kutoa salamu na ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora waliojitokeza. Ndugu Abdallah Shaibu amesisitiza masuala muhimu ikiwemo utunzaji wa mazingira hasa suala la upandaji wa miti, kulinda vyazo vya maji sambamba na utolewaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira. Aidha Ndugu Abdallah amesisitiza kuwa utunzaji wa mazingira utachochea maendeleo ya uchumi wa taifa kama kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, inavyosema “Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa