• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, WILAYANI URAMBO

Posted on: December 1st, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameungana na mamia ya wananchi wa Tabora kushiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kwa ngazi ya Mkoa yanafanyika Wilayani Urambo. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Jamii Iongoeze Kutokomeza UKIMWI”

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili katika viwanja vya Wananchi Squire vilivyopo Wilayani Urambo na kupokelewa na baadhi ya viongozi kutoka Wilaya ya Urambo, tayari kushiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kwa ngazi ya Mkoa yanafanyika Wilayani Urambo.

Baadhi ya wananchi kutoka Wilaya ya Urambo wamejitokeza na kushiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kwa ngazi ya Mkoa yanafanyika Wilayani Urambo, kwenye Viwanja vya Wananchi Squire.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikagua, kujionea na kupata maelezo kutoka kwa wataalamu wa masuala ya Afya kwenye mabanda yaliyokuwepo katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani , yakihusisha wadau mbalimbali wakiwemo MDH.

Baadhi ya wananchi wakijitokeza sehemu za kutolea huduma za afya kwenye mabanda zikiwemo uchangiaji wa damu, upimaji wa VVU, upimaji wa Maralia na utolewaji  w ushauri na nasaa kuhusiana na masuala ya Afya, kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani .

Kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndugu. Joseph Kasiga akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Afya hususani hali ya maambukizi ya VVU Kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Ndugu. Innocent Nsenna Katibu Tawala Wilaya  ya Urambo akitoa salamu za Mkoa na kisha kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwa ajili ya kuwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mahadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia mamia ya wananchi kutoka Wilaya ya Urambo na maeneo ya jirani kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kwa ngazi ya Mkoa yamefanyika Wilayani Urambo, kwenye viwanja vya Wananchi Squire, Disemba 1, 2023.

Ambapo sehemu kubwa ya hotuba yake, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameeleza mafanikio makubwa yaliofikiwa kwenye sekta ya afya kwa kipindi cha miaka miwili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano, hususani ujenzi wa hospitali mpya za wilaya, vituo vya afya, majengo ya dharura na majengo ya wagojwa wenye mahitaji maalumu.

Pia, Dkt. Batilda ameelezea, mwamko wa wananchi wa mkoa wa Tabora katika suala la upimaji wa VVU kwa hiari jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kwa Serikali kuweka mikakati ya kupambana na maambukizi mapya.

Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amebainisha changamoto ya wimbi la vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono ambao wameongeza kasi ya kusambaa kwa maambukizi ya VVU na kuhatarisha maisha ya watanzania. Na kutoa rai kwa watanzania kuendelea kujikinga na VVU kwani bado ugonjwa huu upo.

Wananchi wa Wilaya ya Urambo na maeneo ya jirani wakisikiliza hotuba ya  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian aliyoihutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya Ya Urambo, mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka Wilaya Ya Urambo, mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya Usalama ya Wilaya ya Urambo mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini mbalimbali mbalimbali kutoka Wilaya Ya Urambo, mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani .

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Afya na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kutoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian  akiondoka na kuwaaga wananchi wa Wilaya ya Urambo na maeneo ya jirani  kwenye viwanja vya Wananchi Squire mara baada ya kumaliza kwa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani. ambayo kwa ngazi ya Mkoa yalifanyika Wilayani Urambo, kwenye viwanja vya Wananchi Squire, Disemba 1, 2023.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwa ngazi ya Mkoa yanafanyika Wilayani Urambo wakati huo huo maadhimisho haya kwa ngazi ya taifa yanafanyika Mkoani Morogoro, ambayo yalifunguliwa Novemba 24, 2023.


Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa