• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI SIKONGE NA UYUI

Posted on: November 9th, 2023



Leo Novemba 9, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amefanya ziara wilayani Sikonge na Uyui kwa lengo la kufika na kujionea maeneo yaliotengwa kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi. Akiwa wilayani Sikonge alitembelea hifadhi ya Nyanhua Mbuga na Wilayani Uyui alitembelea hifadhi ya Kigwa- Rubuga.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alipata taarifa kutoka TFS kuhusiana na maeneo yaliotengwa kwa ajili ya makazi ili kuepukana na uvamizi wa  maeneo ya hifadhi. Na kuagiza wasimamizi wa hifadhi kusimamia zoezi zima la uhifadhi wa Mazingira. Ambapo aliwataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kubainishi hatua stahiki zitakazochukuliwa katika mchakato mzima wa ugawaji wa ardhi.

Aidha Mhe. Batilda amewashukuru wataalamu wote waliotoa maoni yao kuhusiana na utengefu wa maeneo hayo ya makazi, na kuyachukua maoni hayo na kuyawasilisha Serikali kuu, ili kuhakikisha zoezi la ugawaji wa maeneo yaliotengwa unakamilika.

Ameongeza kuwa, mchakato wa kuwahamisha wananchi waliovamia hifadhi utashirikisha wananchi kwa kutoa elimu ili kuhakikisha mchakato huo unakamilika pasipo kutumia nguvu.

Mhe. Burian ametoa wito kwa TFS na kamishina wa Ardhi Mkoa wa Tabora  kusimamia zoezi zima la ugawaji wa maeneo ili shughuli za kilimo ziendelee bila kuwakwaza Wananchi.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiongea na wananchi wa Kijiji cha  Msonga, Kata ya Nyanhua alipokuwa kwenye ziara Wilayani Sikonge na Uyui, Novemba 9, 2023.

Mkuu wa Mkoa amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa eneo lenye ukubwa wa Hekta 5000, kwa ajili ya makazi mapya ya wanakijiji wa Nyanhua na Matagata Wilayani Sikonge. Na Hekta 36706 zimetengwa Wilayani Uyui. 

Mhe. Batilda ametoa wito kwa wakazi wa Sikonge na Uyui kuangalia namna nyingine za kuendeleza shughuli za Kilimo badala ya kung’ang’ani mtindo wa kuanzisha mashamba karibu na makazi ili kuhakikisha shughuli za kilimo haziharibu mazingira.

Kamishina wa ardhi Mkoa wa Tabora Ndugu,  Hussein  Sadik Iddi akitoa ufafanuzi wa kina kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian kuhusiana na  hatua zilizochukuliwa wakati wa utengaji wa maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi.

Ambapo kwa upande wa Kamishina  wa Ardhi Mkoa wa Tabora aliwasilisha maelezo ya kina kuhusiana ushirikishwaji na utekelezwaji wa maagizo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusiana na utengaji wa Hekta 5000, kwa ajili ya makazi.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Simon Chacha, akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kuhusiana na hatua ambazo uongozi wa Wilaya umezichukua kuhusiana na uvamizi wa maeneo ya hifadhi pamoja na utengaji wa maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Kata ya Nyanhua.

 Mhe. Chacha ameleeza kuwa, kuna haja ya kuimarisha doria ambazo zitakuwa zinafanywa mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi hawafanyi uvamizi kwenye hifadhi zetu.

Na kupitia maagizo yaliotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari Wilaya imeshatenga maeneo kwa ajili ya makazi mapya. Na pia amemuhakikishia kuwa, wananchi wapo tayari kuhama na  kwenda sehemu zingine.

Mhe DC amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga eneo Hekta 5000, kwa ajili ya  makazi mapya na kama uongozi wa wilaya yupo tayari kutekeleza maagizo.

Kuna haja ya kufahamu idadi ya watu, ila kwa kuwa mkuu wa mkoa ameshatoa maelekezo tunatahakikisha tunafika na kuonana na viongozi wa vijiji ili kuwatambua wakazi waliopo ili kurahisisha zoezi la ugawaji wa ardhi linakamilika.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakaria Mwansasu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kuhusiana na hatua ambazo uongozi wa Wilaya umezichukua kuhusiana na uvamizi wa maeneo ya hifadhi pamoja na utengaji wa maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Kata ya Kigwa, Wilaya ya Uyui.

Mhe. Zakaria ameeleza hatua zilizochukuliwa kutokana na maagizo ya Mhe. Rais kuhusiana na kutenga maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi. Ambapo kwa wilaya ya Uyui jumla ya Hekta 36,706 zimetengwa kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi na tayari mchakato wa kugawa maeneo umeshaanza.

Aidha Mhe. Zakaria amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga eneo Hekta 18,353 kwa ajili ya makazi na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Uyui.

Kwa niaba ya Meneja wa TFS Kanda ya Magharibi Kamanda Aloyce Kilemwa akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, kuhusiana maeneo yaliotengwa na hatua ambazo TFS imezichukua katika kuhakikisha utengaji wa maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli unakamilika bila kuathiri utunzaji wa mazingira. 

Utoaji wa ufafanuzi ulienda sambamba na usomwaji wa ramani inayoonesha ugawanyo wa maeneo ya hifadhi na makazi ya watu. 








Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa