• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA ATEMBELEA MIRADI YA SEQUIP WILAYANI IGUNGA

Posted on: November 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule wa Sekondari ya Tambalale na Shule ya Sekondari Mtungulu, zilizopo, Wilayani Igunga, ikiwa ni sehemu ya miradi 14 ambayo inakamilishwa kupitia program ya SEQUIP.

Kupitia ziara hiyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amemshukuru na kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kukamilisha miradi ya shule ambayo inawafikia wananchi wengi hususani wa vijijini.

“Kwa Kweli nampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha nyingi ambazo zinajenga shule mpaka maeneo ya vijijini, tofauti na hapo awali” alisema Mkuu wa Mkoa

Pia Mhe. Batilda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mhe. Sauda Mtondoo, kuhakikisha anashirikiana na watendaji wengine kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na viwango vinavyotakiwa. Na kusimamia matumizi bora ya fedha ili kuepuka sitofahamu.

“Nitoe wito kwa Mhe.DC hakikisha unashirikiana  na watendaji wako ili miradi hii inakamilika kwa wakati na kusimamia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa na Serikali.” alisema Mhe. Batilda

Magizo hayo yalienda sambamba na pongezi ambazo Mhe. Mkuu wa Mkoa alizitoa kwa wasimamizi wa miradi yote ya SEQUIP inayokamilishwa Wilayani Igunga, hususani uwekwaji wa Kambi za mafundi ambazo zimechangia kasi ya ujenzi.

“Nitoe pongezi kwa Mhe.DC na wasimamizi wote kwa kusimamia miradi hii hasa uwekwaji wa kambi za mafundi ambazo zimechangia kasi ya ujenzi” Aliongeza Mhe. Batilda

  • Pia ameziagiza kamati za ujenzi kufanya kazi usiku na mchana na kuwa wakali kwa wafundi, kuongeza ufanisi na ubunifu katika usimamizi wa miradi yote ya Serikali.

“Naziagiza kamati za ujenzi kuhakikisha wanakuwa wakali kwa mafundi na kufanya kazi kwa ubunifu na ufanisi ili kukamilisha miradi hii kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa”

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mhe. Sauda Mtondoo, amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, maagizo aliyoyatoa   wameyapokea na kuyatekeleza kikamilifu na  kusimamia miradi hiyo   kikamilifu.

“Maagizo yaliotolewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa tumeyapokea, na sisi kama viongozi wa Wilaya tutahakikisha maelekezo yote tuliopewa tunayafanyia kazi na kukamilisha miradi hii kwa wakati na viwango vinavyotakiwa” Alisema Mhe.DC

Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi, Ndugu.Mihambo Msayu amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, kuyatekeleza maagizo waliopewa na kusimamia miradi ya shule  usiku na mchana mpaka kukamilika kwake.

Kupitia program ya SEQUIP Mkoa wa Tabora utakamilisha miradi ya shule Mpya za sekondari kumi na nne (14) ambazo mpaka kukamilika kwake itagharimu shilingi Bilioni 8.4. ambapo kila mradi umepangwa kugharimu shilingi Milioni 603.8.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa