Kufuatia kumiminika kwa miradi mingi ya maendeleo Moan Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameungana na Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa miaka miwili ya uongozi wake Mkoa umefanikiwa kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Miundombinu ya barabara na maji, ujenzi wa reli ya kisasa na maboresho ya miundombinu ya elimu. Sambamba na hilo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati safi kwa miaka miwili mfululizo.
Aidha ameitaka Halmashauri hiyo kuangalia namna mpya ya utoaji na ufuatiliaji wa mikopo ya asilimia 10, ambapo bado kuna changamoto ya urejeshaji wa mikopo hiyo na kuleta changamoto kwa Halmashauri. Sambamba na hilo bado kuna changamoto ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia mfumo wa TAUSI ambao unasafanya kazi sambamba na mashine za POS ambapo ripoti inaonyesha bado kuna changamoto ya usajili na matumizi yake.
Pia amewakumbusha watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa. Sambamba na kusimamia suala la maadili kwa watoto hasa kipindi hiki ambacho taifa linakumbana na suala la ushoga.
Haya yamejili leo Juni 10, 2023 wakati Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian alipohudhuria Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Tabora cha kupokea taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyoishia Juni 30, 2022.
________________________
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa