• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AWAHIMIZI WAFANYABIASHARA MNADANI IPULI KUCHUKUA TAHADHARI YA KUJIKINGA NA COVID 19

Posted on: June 28th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wananchi na wafanyabiashara katika Mnada wa Ipuli kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona(COVID-19)

Alisema ikiwa nchini jirani zinakabiliwa na tatizo hilo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Tanzania akachukua hatua za kujikinga kama zinavyoshauriwa na wataalamu wa sekta ya afya.

Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo alipokuwa katika ziara ya kukagua ukusanyaji wa mapato na hatua zinazochukuliwa kwa wafanyabiashara wa ng’ombe , mbuzi na kondoo katika Mnada wa Ipuli uliopo Manispaa ya Tabora za kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

Alisema ni lazima kwenye Minada  na maeneo yanayokusanya watu wengi kama vile masokoni , Stendi ,mashuleni kukawekwa ndoo za maji tirikia , sabuni ili wanaofanya shughuli hapo waweze kunawa kila wakati.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza watu wote wanaoendesha shughuli za kujitafutia riziki katika Mnada wa Ipuli na maeneo yenye mikusanyiko kuvaa wakati wote barakoa  na kutumia vitakasa mikono.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa  Mkoa ameiagiza Idara ya Afya ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha inajenga vyoo na kuboresha hali ya usafi katika Mnada wa Ipuli ili kulinda afya za watu wanakwenda siku ya Jumamosi kupata nyama choma.

Alisema ya usafi katika Mnada huo hairidhishi na vyoo vilivyopo ni vichache ukilinganisha ya watu wanaokuwepo siku ya Jumamosi.

Aidha Balozi Dkt. Batilda aliwaahidi wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo la baadhi ya watu kuziba njia ya kupeleka ng’ombe mnadani , ukosefu wa majosho, ukosefu wa nyasi za kisasa za kulisha mifugo na ukosefu wa mbegu bora za ng’ombe

Awali mfanyabiashara wa ng’ombe Haruna Mazoea alisema  wamelazima kufuata ng’ombe wa mbegu kutoka Biharamulo mkoani Kagera na wengine nchini Rwanda kama njia ya kuboresha ng'ombe wa Tabora.

Alisema aina ya ngo’mbe kutoka Biharamulo wanafaida kwa kuwa ni wakubwa na  wanauzwa kuanzia shilingi milioni 1.8 hadi 2 kwa mmoja.

Mazoea aliiomba Serikali kuasaidia kuboresha aina ya ng’ombe Mkoani Tabora kwa kuwapa wafugaji mbegu bora za ng'ombe na kuwapatia mbegu za majani kupanda kwa ajili kulisha na kunenepesha mifugo wao ili waweze kupata bei kubwa.

Mkuu wa Mnada wa Ipuli katika Manispaa ya Tabora Freddy Newton alisema siku ya mnada wanapokea kati ya ng'ombe 200 hadi 250 na mbuzi 100 hadi 150.

Alisema ng'ombe mmoja analipiwa ushuru wa shilingi 7,500/= na mbuzi 3,000/= ambapo Manispaa ya Tabora inachukua kwenye fedha hizo shilingi 1,500/= kwa ng'ombe na 500/= kwa mbuzi anayeuzwa.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Tabora ni mwendelezo wa ziara ambazo amezipanga za kukutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitatua ili kujenga Tabora mpya.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa