Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian Leo Julai 18, 2023 amefungua semina ya uelimishaji wa Umma kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwanakiyungi.
Akitoa hotuba yake, amewataka watalaamu ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao.
“Ni imani yangu kwamba zoezi hili litasaidia kujenga uelewa kwa viongozi wote, hivyo mnapaswa kushiriki kikamilifu katika semina hii kwa lengo la kupata uelewa”
Sambamba na hilo, ametoa wito kwa washiriki kuhakikisha elimu hii inawafikia wadau wote wa maendeleo ili kuhakikisha Dira ya maendeleo ya 2050 inagusa watu wote.
“Ninatarajia kutakuwa na ushirikishwaji mpana wa wadau wote katika ngazi zote ikiwemo taasisi za elimu ya juu, sekta binafsi na Asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla”
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa