Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema kuwa, anamshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya kwa kuendelea kutenga fedha ambazo zinaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ununuaji wa zana za usafirishaji.
“Rais wetu kipenzi ameamua kutoa kiasi cha Shilingi milioni 934.5 kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa vyombo vya usafiri ikijumuisha magari 5 yenye thamani ya Shilingi milioni 802.4 na pikipiki 48 zenye thamani ya Shilingi milioni 132 zitakazoenda kuongeza nguvu katika usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji katika Mkoa wetu” alisema Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hilo, Mheshimiwa Batilda ametoa wito kwa wadereva wa Vyombo hivyo kufuata Sheria kikamilifu ili kuepukana na ajali.
“Madereva wa magari na pikipiki waendeshe kwa kufuata sheria za barabarani ili kuepuka kupata ajali ambazo zinaweza kutokea kama sheria za barabarani hazitofuatwa” alisisitiza Mhe. Batilda
Naye, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tabora Muhandisi Hatari Kipufi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili na nusu huduma za maji mkoani Tabora zimeimarika kwa kiasi kikubwa sana ambapo kwa upatikanaji wa maji mijini ni asilimia 75 na vijijini ni asilimia 68 ambapo mpaka kufikia mwaka 2025 upatikanaji wa maji mjini unatarajiwa kufikiwa asilimia 95 na vijiji ni asilimia 85.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora amekabidhi magari matano kwa watendaji wa RUWASA, ambapo gari moja amekabidhiwa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tabora na mengine manne wamekabidhiwa Mameneja wa RUWASA wa wilaya ya Igunga, Nzega, Uyui na Sikonge.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili karika Ofisi ya RUWASA Mkoa wa Tabora, iliyopo Manispaa ya Tabora kushiriki kwenye hafla ya ugawaji wa vyombo vya usafiri kwa watendaji mbalimbali wanaohudumu kwenye selta ya maji ikihusisha magari matano (5) na pikipiki arobaini na tano (45) Januari 10, 2024.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tabora Muhandisi Hatari Kapufi akitoa taarifa ya maendeleo ya Sekta ya maji Mkoani Tabora kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwenye hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Ndugu Hassan Wakasuvi, Katibu wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu. Emmanuel Sabuhoro akitoa salamu za Chama Chama cha Mapinduzi katika hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia watumishi wa RUWASA, Jumuhiya za Watumiaji Maji, Wadau wa Sekta ya Afya na Wananchi katika hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikata utepe kuashiria kukamilika kwa hafla ya ugawaji wa vyombo vya usafiri kwa watendaji mbalimbali wanaohudumu kwenye Sekta ya maji ikihusisha magari matano (5) na pikipiki arobaini na tano (45) Januari 10, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi gari jipya aina ya Land Cruiser Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tabora Muhandisi Hatari Kapufi kwenye hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwakabidhi funguo za magari na pikipikiMameneja wa RUWASA wa Wilaya kwenye hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwakabidhi funguo za pikipiki baadhi ya viongozi wa Jumuhiya mbalimbali za watumiaji maji kwenye hafla fupi ya ugawaji wa vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA zilizopo Manispaa ya Tabora, Januari 10, 2024
Haya ndio magari matano (5) na pikipiki arobaini na tano (45) ambazo leo Januari 10, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amezigawa kwa watendaji wa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa