• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA “NENDA KACHAPE KAZI, MHE. RAIS AMEKUAMINI”

Posted on: October 4th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, amemuagiza Mkuu wa Wilaya Urambo Mhe. Eribariki Bajuta kwenda kufanya kazi na kuwatumikia wanaurambo kwani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemuamini na kumpatia nafasi hiyo. Ameyasema hayo leo Oktoba 4, 2023 alipokuwa akimuapisha Mkuu wa Wilaya huyo kwenye Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

 

Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa amemtaka DC. Bajuta kusimamia amani ambayo ni tunu kwa Watanzania na Urambo kwa ujumla ili kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

 

“Ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, hakikisha unasimamia Amani na Utulivu katika Wilaya yako ili wananchi wapate fursa ya kujishughulisha na kazi za maendelo ili wapate vipato na kupunguza umasikini” Alisema Mhe. Batilda 

 

Pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya wa Urambo kwenda kusimamia maslahi ya wakulima hususani suala zima la madeni ambayo yamekuwa kero kwa wakulima wa zao la Tumbaku  Wilayani Urambo.

 

“Wananchi wa Wilaya ya Urambo ni wakulima wa mazao ya Chakula na Mazao ya biashara hususani Kilimo cha Tumbaku, hivyo ukasimamie kuhakikisha Madeni ya wakulima wa Tumbaku yanalipwa na Vyama vya Ushirika” alisisitiza Mkuu wa Mkoa.

 

Aidha Dkt. Batilda amemuagiza DC. Eribariki Bajuta kushirikiana na watendaji wa serikali wa ngazi zote ili kuhakikisha wanawatumikia wananchi wa Urambo ambao wanategemea kwa kiasi kikubwa miradi ya maendeleo inayoletwa na Serikali.

 

“Kasimamie Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ili iwatumikie wananchi kwani Halmshauri zinapewa fedha nyingi za kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi” Alisema Dkt. Batilda 

Mbali ya hayo Mhe. Mkuu wa Mkoa alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Urambo kusimamia mambo kadha wa akdha yakiwemo, suala la utunzaji wa mazingira, kufanya mikutano ili kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi na pia kuendeleza baadhi ya mambo yaliokuwa yakifanywa na mtangulizi wake.

 

Mhe. Eribariki Saimon Bajuta anakwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo, kuchukua nafasi ya Mhe. Kenani Kihongosi ambaye anakwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa