Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amefanya ziara katika Bwawa la Igombe lilipo Manispaa ya Tabora na kuridhishwa na kasi ya ukarabati wa Bwawa hilo, ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2023 alipofanya ziara Bwawani hapo.
“Kwa hakika nimeridhishwa na kasi ya ukarabati wa bwawa hili, na kuonyesha thamani ya fedha ilitolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.” Alisema Dkt. Batilda.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa viongozi ngazi ya Wilaya, kata na vijiji pamoja na wananchi walio jirani na bwawa hilo kutunza mazingira ili kuokoa vyanza vya maji na kuhakikisha Mkoa unakuwa na maji ya uhakika kwa wakati wote, licha ya Mkoa kupata maji Ziwa Victoria.
“Napenda nitoe wito kwa viongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya , kata na vijiji Pamoja na wananchi waliopo Jirani, kuhakikisha wanalinda bwana hili ambalo limekuwa msaada mkubwa sana kwetu licha ya kwamba tunapata maji kutoka ziwa Victoria.” Alisema RC. Batilda
Aidha ametoa pongezi kwa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Tanganyika na TUWASA kwa kusimamia vema ukarabati wa bwawa hilo na kuboresha huduma ya maji safi na salama.
“Napenda kutoa shukrani na pongezi zangu kwa wasimamizi wote wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Tanganyika na TUSAWA kwa kusimamia ukarabati huu na sasa wananchi wa Tabora wanakwenda kupata maji safi na salama.” Alisema Dkt. Batilda.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Peter Bura amehaidi kusimamia na kutekeleza maagizo yote aliyopewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ili kuhakikisha bwawa hilo linakuwa na tija kwa wananchi.
“Kama Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alivyoelekeza, sisi kama wasimamizi wa Wilaya tutahakikisha tunasimamia na kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa ili kuhakikisha bwawa hili linakuwa salama na kutoa huduma ya maji kwa uhakika.
Mpaka kukamilika kwake, mradi huu wa ukarabati wa Bwawa utakuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 1.5, fedha kutoka Serikali kuu kupitia Wizara ya Maji, ambazo awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian aliziomba kwa Waziri wa Maji Mhe. Juma Awaso alipofanya ziara Mkoani Tabora mwaka 2022.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa