Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian amewahakikishia wakulima wa tumbaku Mkoani Tabora kuwa, Serikali yetu ni sikivu na inachukua hatua za haraka pale changamoto zinapojitokeza. Na kuwataka viongozi hao kuwa watulivu wakati Serikali ikiangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Ameyasema hayo leo Julai 12, 2023 alipokutana na baadhi ya wawakilishi wa vyama vya msingi (AMCOS) vya wakulima wa Tumbaku Mkoani Tabora kwenye ukumbi mdogo uliopo ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora.
Dkt. Batilda ameeleza kuwa, Serikali inatambua kuwa, bado kuna baadhi ya wakulima hawajalipwa fedha zao licha ya kuuza Tumbaku kwa makampuni yanayohusika.
“Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wakulima wa tumbaku hususani suala la ucheleweshwaji wa malipo yenu, na sisi kama Serikali kwa kushirikiana na makampuni ya ununuzi wa Tumbaku pamoja na taasisi za fedha, kuona kwa namna gani tunatatua changamoto hii haraka iwezekanavyo, kwa sasa Banki zinakabiriwa na uhaba wa “Dollar” na hivyo tunaangalia namna nzuri ya kuhakikisha wakulima wanapata malipo yao.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewaomba wakulima Mkoani Tabora kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto hii ya uchelewashwaji wa malipo.
“Niwaombe wakulima wetu muendelee kuwa watulivu huku Serikali kwa kushirikiana na makampuni husika na taasisi za kifedha kuhakikisha wakulima wote mnapata malipo yenu kwa wakati.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa