Kufuatia makosa ya kijinai na kinidhamu yaliofanywa na mtumishi Ndugu, Rayson Agenelus Duwe ambaye ni Muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge, anatuhumiwa kufanya kosa la kumwingilia kimwili mgonjwa aliyekuwa amelazwa Hospitalini aliyefahamika kwa jina (limeifadhiwa) mwenye Umri wa miaka 18 Kabila lake Msukuma, akiwa ni Mjamzito wa wiki 32.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameleza kuwa amesikitishwa na tukio hilo na Serikali ngazi ya Mkoa imeamua kuchukua hatua ya kuunda timu ya uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kuchukua hatua za kinidhamu za Utumishi na kuangalia hali halisi ya utendaji kazi katika Hospitali kwa ujumla.
Haya ameyasema leo June 14, 2023,wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi mdogo uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Ambapo mpaka sasa hatua za awali za kumkamata na kumfungulia mashtaka mtuhumiwa huyo zimefanyika na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili. Hadi hivi sasa Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakama.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa