Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Balozi Batilda Salha Burian amelitaka Baraza la Madiwani Halmashauri ya Uyui kuhakikisha malipo na makusanyo yote yanayohusu fedha za serikali yapitie kwenye mfumo rasmi wa serikali ili kuhakikisha mapato na matumizi ya serikali yanasimamiwa kikamilifu.
Aidha amelitaka baraza hilo kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na kamati za Bunge ili kuhakikisha Halmashauri inatimiza wajibu wake. “bado kuna utekelezaji hafifu wa Maagizo ya kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC). Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ilipewa maagizo matatu (3), ambapo maagizo yote matatu (3) bado yanaendelea na utekelezaji”, alisema Dkt. Batilda Burian
Haya yamejili leo Juni 9, 2023 wakati Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian alipohudhuria Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Uyui cha kupokea taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyoishia Juni 30, 2022.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa