Alisema “Matokeo ya SENSa ya watu na makazi, SENSA ya majengo na SENSA ya anuani za makazi yawe ndio dira yetu inayotuongoza katika kuandaa na kuhuisha sera, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango na program za maendeleo ya mkoa wetu na kutathmini utekelezaji wake”
Sambamba na hilo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa, kupitia SENSA ya watu na makazi ya mwaka 2022, mkoa wa Tabora una idadi ya watu wapatao milioni 3.3 ambapo wanawake ni milioni 1.7 na wanaume ni milioni 1.6 na kuufanya mkoa wa Tabora kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa kuwa na idadi kubwa ya watu.
Aidha, Mhe. Batilda Burian amebainisha malengo ya mafunzo hayo kuwa ni kujenga uwezo wa kutafsiri, kuchambua na kuyatumia matokeo ya SENSA katika mpingo mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kuwa “kwa kuwa suala la kupanga mipango ya maendeleo ni shirikishi na linaanzia ngazi ya chini hadi taifa, sisi kama viongozi tuna wajibu wa kuratibu suala zima la upangaji wa maendeleo katika mkoa wetu”
Naye, Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ndugu. Benedict Mugambi amesema kuwa mafunzo haya yanalengo ya kuwajengea uwezo viongozi wa kiserikali na makundi mbalimbali katika kupanga mipango ya maendeleo kwa kutumia taarifa rasmi zilizopo kwenye matokeo ya SENSA mbalimbal zilizofanyika.
Mfunzo haya ya matumizi ya matokeo ya SENSA ya watu na makazi ya mwaka 2022 yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Peter Bura asubuhi ya leo Januari 18, 2024 na yalihusishwa viongozi mbalimbali wa serikali kuanzia kazi ya kata hadi mkoa sambamba na wananchi kutoka kwenye makundi mbalimbali. Mafunzo haya yanafanyika kwa awamu, ambapo kwa mkoa wa Tabora awamu ya kwanza imeanzia wilaya ya Tabora na kumalizikia wilaya ya Uyui Januari 19, 2024.
Mafunzo haya yalienda sambamba na ugawaji wa ramani zenye taarifa kuhusiana na idadi ya watu na makazi ambazo ziligawiwa kwa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi ngazi ya kata.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ndugu. Benedict Mugambi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, ramani ya Mkoa wa Tabora yenye kuonyesha makazi ya watu na idadi yao mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuhutubia kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya SENSA ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali kutoka Mkoani Tabora, yaliofanyika katika ukumbi wa Ristalemi, Januari 18, 2024
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Ramani zenye kuonyesha makazi na idadi ya watu mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuhutubia kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya SENSA ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali kutoka Mkoani Tabora, yaliofanyika katika ukumbi wa Ristalemi, Januari 18, 2024
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora, Ramani zenye kuonyesha makazi na idadi ya watu mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuhutubia kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya SENSA ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali kutoka Mkoani Tabora, yaliofanyika katika ukumbi wa Ristalemi, Januari 18, 2024.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwakabidhi Watendaji wa Kata wa Manispaa ya Tabora Ramani zenye kuonyesha makazi na idadi ya watu mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuhutubia kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya SENSA ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali kutoka Mkoani Tabora, yaliofanyika katika ukumbi wa Ristalemi, Januari 18, 2024.
Mkuu wa Mkoa amegawa Ramani hizo kwa Watendaji wote wa Kata ishirini na Tisa (29) zilizopo Manispaa ya Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa