Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanawapatia watoto lishe bora ili kuhakikisha watoto wanakuwa na afya njema wanapokuwa nyumbani na shuleni. Ameyasema hayo leo Julai 14, 2023 alipofanya ukaguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ipumbulya, kata ya Bukoko wilayani Igunga.
Dkt. Batilda amesema kuwa “Mkoa wa Tabora umebarikiwa kuwa na ardhi ambayo inastawisha mazao mengi ya chakula, na hivyo hakikisheni mnalima mazao ya kutosha ili kuwa na uhakika wa lishe bora kwa watoto wetu waliopo shuleni, ili tuondokane na changamoto ya chakula mashuleni, ili kwenda na kasi ya maboresho ya miundombinu yanafanywa na Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Sambamba na hilo Dkt. Batilda Burian amewapongeza wakazi wa kijiji cha Bukoko kwa kujitolea kwa hali na mali katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ambao umefikia kwa asilimia 75.
“ nipende kuwapongeza kwa kujitoa na kufikia hatua hii ya ujenzi ambayo kwa hakika unaeidhisha, sisi kama Serikali tutahakikisha tunawajibika kwa nafasi yetu kuhakikisha Zahanati hii inakuwa na vifaa na wahudumu” alisema Dkt. Batilda
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa