Leo Julai 22, 2023 kwenye Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi Madereva wa Serikali na baadhi ya wadau wa Usalama Barabarani wamehudhuria Semina elekezi iliyotolewa na Chama Cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) yenye malengo ya kuwakumbusha madereva na wadau hao mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutimiza majukumu yao ya Kiserikali.
Ndugu Elihuruma Javan Nyella Afisa Utumishi Mkuu (M) Tabora ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya amewakumbusha na kuwataka madereva hao kuzingatia sheria za barabarani, kujiendeleza kitaaluma, kufuata maadili ya utumishi wa Umma, Kujiheshimu na kuwaheshimu wengine na Kupima afya mara kwa mara, ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo.
Aidha, Ndugu Elihuruma Javan Nyella amewaeleza madereva hao kuwa, Serikali inatambua mchango wao katika kufanikisha na kutekeleza shughuli mbalimbali za kiserikali Mkoani Tabora, na kwa kutambua hilo Serikali itahakikisha inaweka mazingira mazuri kwa madereva wa Serikali ili waweze kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa