Mbunge wa Jimbo la Ulyankuru, Mhe. Rehema Migilla amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani imefanikiwa kuweka mazingira mazuri ya mwanamke kuweza kujitegemea na kuondokana na mifumo ya utegemezi iliyozoeleka hapo awali. Ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo yalifanyika wilayani Kaliua.
Mhe. Reheme amsema kupitia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yalioazishwa na serikali kuanzia ngazi ya mkoa hadi kata yamekuwa msaada kwa wanawake, kwa kuanzisha shughuri mbalimbali za kiuchumi.
Aidha Mhe. Migilla amewataka wanawake kujitokeza na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, ili kuhakikisha wanawake wanashiriki kwenye mipango mbalimbali ya serikali kupitia serikali za mitaa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa