Kufuatia mgomo wa wafanyabishara ulitokea leo Julai 3,2023 Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Rashid Chuachua amewataka wafanyabiashara Mkoani Tabora kuisaidia Serikali katika kupambana na vitendo vya Rushwa kwani serikali haiungi mkono vitendo vya rushwa. Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian alieleza kuwa Serikali haitakumbatia wala rushwa na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara hao kutoa taarifa kwa TAKUKURU, na Serikali itahakikisha inawalinda wote wanaotoa ushirikiano katika jitihada za kupambana na rushwa.
Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa mamlaka ya ukusanyaji wa mapato TRA kutokufunga biashara pasipo kufuata utaratibu “Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora napiga marufuku vitendo hivi” alisema Dkt Chuachua. Ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita itahakikisha inawachukulia hatua watendaji wote wanaokiuka taratibu za ukusanyaji wa wapato.
Akijibu maswali yalioulizwa, Dkt Chuachua amewaomba wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huo na kuendelea na shughuli zao za kibiashara na tayari Serikali imeshachukua hatua za kuwasimamisha kazi wafanyakazi wawili wa TRA huku uchunguzi ukifanyika kufuatia tuhuma za ukiukwaji wa utaratibu wa ukusanyaji wa mapato.
Naye ndugu Shabani Ramadhani kwa niaba ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Tabora, ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuchukua hatua za haraka na kutatua changamoto za wafanyabiashara. Na hivyo wameridhika na majibu waliopewa na Serikali na wapo tayari kuendelea na shughuli zao. Wafanyabiashara Mkoa wa Tabora tunamuunga mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha tunalipa kodi ipasavyo” alisema.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa