• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

SERIKALI YATAKIWA KUTOWAONEA AIBU WANAOLETA MZAHA JUU YA UGONJWA WA COVID -19

Posted on: April 3rd, 2020

VIONGOZI  wa Dini  Mkoani Tabora wameiomba Serikali kutowaone aibu wale wote wanaoleta mzaha na wanaotafuta umaarufu kupitia janga la ugonjwa wa homa  kali ya mapafu unaoeneza na kirusi kipya aina ya Corona Covid-19.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia nzima mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.

Mchungaji wa Kanisa la Agape Miracle Centre Elias Mbagata alisema bado kuna kuna mizaa inaendelea juu ya janga hili hivyo ameiomba serikali isiwaonee haya wanoendekeza hayo hata kama ni viongozi wakubwa wakiwemo wa Dini.

Alisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuwajengea matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu ambayo itawasababisha wachanganyikiwe.

Askofu wa wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora, Dk Elias Chakupewa alisema wameshachukua hatua mbalimbali za kuwaelimisha waumini wao kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo maelekezo ya wataalamu na viongozi wa Serikali namna sahihi ya kujikinga na janga la Covid -19.

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka aliwaomba waumini kuungana na serikali katika kupigana vita hii iliyo mbele yao kwa kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi pamoja na wataalam wa afya.

Alisema Kanisa hilo limesitisha kwa muda baadhi ya taratibu za uendesha wa Ibada ikiwa ni seehemu ya mikakati ya kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya Covid -19.

Kwa upande wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi aliwashauri viongozi wa Dini kuendelea kushirikiana na serikali na kufuata maelekezo ya wataalamu katika kuhakikisha wananchi na waumini wao wanapata maelekezo sahihi kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo hatari.

Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Magharibi Ezekiel Yona alisema wao kwa kutambua ukubwa wa tatizo wametoa jingo katika Hospitali yao ya Sikonge kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Covid -19 kama kwa bahati mbaya wataonekana.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati, Askofu Isaac Laizer alimpongeza Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa  kwa kuthubutu kuitangazia dunia kwamba janga la ugonjwa wa Corona litamalizika kwa wananchi watakapokubali kumuomba Mungu.

Alisema wao wanaungana na Serikali kwa kusimamisha baadhi ya huduma ikiwemo ya mafunzo kwa watoto wadogo (Sunday school) na kualika wataalamu kutoa elimu ya kujikinga na Corona.

Viongozi hao wamadhehebu ya dini wamesema kwamba pamoja na serikali kuchukua taadhali inabidi wananchi kumlilia Mungu ili awasamehe dhambi na kuwaepusha na janga hilo.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwashukuru viongozi hao wa kiroho kwa ushirikiano wanaotoa kwa Serikali na kuwaomba wasaidie kufikisha elimu kwa waumini wao ili isaidie kuuepusha Mkoa huo na janga la Covid 19.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa