Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na mlezi wa Mkoa wa Tabora Muhandisi Nasri Ally amewaongoza mamia ya wanachama kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora kushiriki kwenye maadhimisho ya miaka arobaini na saba (47) ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi yaliofanyika katika Uwanja wa Kilimba, Wilayani Kaliua Februari 4, 2024.
Akihutubia mamia ya wanachama waliojitokeza. Muhandisi Ally amewataka wanachama wa Chama cha mapinduzi kuendelea kuyaishi maisha ya wasisi wa chama hiko huku akisisitiza umoja na mshikamano ndani ya chama.
Aidha, Muhandisi Nasri amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vema chama hiko na kutekeleza Ilani ya CCM kwa kasi kubwa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amesema kuwa, kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoa wa Tabora Ilani imetekelezwa kwa kiasi kikubwa sana huku akitaja miradi mikubwa ya elimu na Afya ambaye imekamilishwa mkoani Tabora.
Ikumbukwe kuwa, maadhimisho ya miaka arobaini na saba (47) ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliofanyika katika uwanja wa Kilimba, Wilayani Kaliya Februari 4, 2024
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa