Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tabora Bwan. Venance Msafiri amewaongoza wenyeviti na watendaji wakuu kutoka kwenye vyama vyote vya ushirika (AMCOS) vilivyopo mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Majukwaa ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika unaotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 29, 2024 na kumalizika Aprili 30, 2024.
Bwan. Msafiri amesema kupitia wizara ya kilimo serikali imependekeza kuanzishwa kwa majukwaa hayo kwa ajili ya kujadili mambo kadha wa kadha kuhusiana na maendeleo ya vyama vya ushirika mkoani Tabora na Tanzania kwa ujumla ili kuwapa wakulima nafasi ya kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo kwenye ushirika.
Aidha Bwana. Msafiri ameongeza kuwa, majukwaa hayo yatawapatia wanachama nafasi ya kujadili changamoto na mafanikio yatokanayo na vyama vya ushirika kwani majukwaa hayo yanahusisha wanachama halali kutoka kwenye kila chama cha ushirika.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa