• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TABORA YAJIPANGA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO

Posted on: November 1st, 2023

Meneja wa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Magharibi Ndugu. Omar Wazir Omari akitoa taarifa ya Utabiri wa Hali ya Mvua kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Lois Peter Bura amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria kikao hiko Leo Novemba, 1 2023 Katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

 

Ndugu Wazir ameleza kuwa,

“Utabiri unaonyesha kuwa, mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa kunyesha katika mkoa wa Tabora na zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba 2023 na kuisha kati ya wiki ya tatu na ya nne ya mwezi April 2024.”

 Aidha Ndugu Wazir ameongeza kuwa,

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa, utabiri tulioutoa unaonyesha kuwa Kipindi cha nusu ya kwanza ya msimu ambacho ni kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari, 2024 kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi ikilinganishwa na nusu ya pili ya msimu ya kipindi kinachoanzia mwezi Februari hadi Aprili, 2024.”

 

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya akitoa ufafanuzi kuhusiana na hatua za awali zilizochukuwa na uongozi wa Mkoa wa Tabora kabla ya kupokea taarifa ya Utabiri wa Mvua za simu iliyotolewa na Meneja wa Mamlaka ya Hari ya Hewa Kanda ya Magharibi, iliyotolewa Leo Novemba, 1 2023 Katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

 Dkt. Mboya ameeleza kuwa, 

“Mkoa tunampongeza Meneja Kanda ya Magharibi kwa kuwasilisha taarifa, baada kupokea taarifa hiyo tulikubaliana na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tuite Wadau wachache kuwawakilisha wengine ili kuwajulishwe kwa kina kuhusu taarifa hiyo. Pia tulikubaliana kuita Vyombo vya Habari kuwajulisha kuhusu taarifa hiyo ili wananchi wote wapate taarifa.”

 Dkt. Mboya amesema kuwa,

“Tumewaita baadhi yenu mkiwa sehemu ya wadau ili tuweze kupokea taarifa muhimu za utabiri wa hali ya hewa  kwa kipindi cha miezi 3 ijayo hasa ukuzingatia ndio kipindi cha mvua katika Mkoa wetu. Tunaamini taarifa hizi tutakazozipokea zitaweza kuwafikia wadau wengine ambao hawakuweza kufika hapa na wananchi kwa ujumla ukizingatia kuwa Wanahabari ambao ni wadau muhimu katika kufikisha taarifa hizo kwa haraka wapo hapa. Tunaamini kwa njia mbalimbali za habari wananchi na wadau wote watazipata.”

 

Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Lois Peter Bura akitoa neno wakati wa kupokea taarifa ya Utabiri wa Mvua za simu iliyotolewa na Meneja wa Mamlaka ya Hari ya Hewa Kanda ya Magharibi, iliyotolewa Leo Novemba, 1 2023 Katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

 DC Bura amefafanua kuwa,

“Serikali inaendeleza juhudi mbalimbali katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na yale ya tabia nchi ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari zinazoweza kutokea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Aidha, Serikali imekuwa ikifungua vituo vya mauzo ya mahindi ya bei nafuu kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa wananchi wanaoathiriwa na ukame na kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha. Katika msimu wa Kilimo uliopita zaidi ya tani 4,000 za mahindi ziliuzwa kwa wananchi.”

 

Mhe. DC Ameongeza kuwa, 

Aidha, Mkoa kwa kushirikiana  na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika umekuna na makampuni ya bima na Taasisi za kifedha  ili kuandaa mpango wa pamoja wa bima ya tumbaku Mkoa wa Tabora itakayoenda kutatua na kupunguza athari na majanga ya mvua za mawe. Tayari kikao cha awali kimefanyika kwa ajili ya kujadili bima katika zao la tumbaku na makampuni ya bima yameungana kwa ajili ya bima katika zao la tumbaku. 

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa