• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TABORA YAJIPANGA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Posted on: January 9th, 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameeleza kuwa, Mkoa wa Tabora umejipanga kikamilifu kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu amba kwa siku za karibuni umeonekana kuanza kusambaa. Ameyasema hayo leo Januari 9, 2024 alipokuwa akisoma taarifa kuhusu hali ya Ugojwa huo kwenye kikao cha kamati ya msingi ya mkoa cha kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu.

Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa, Serikali ngazi ya Mkoa itaendelea kupokea taarifa  kutoka Wizara ya Afya kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu ili kuhakikisha Jamii inapata taarifa kamili kuhusiana na ugojwa huo ambao tayari umeshaanza kulipuka nchi za jirani.

“Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini , Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutoa taarifa na takwimu za kuwepo mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu  kuanzia mwezi Septemba 2023 katika baadhi ya nchi jirani kama vile Msumbiji na Zambia pamoja na baadhi ya Mikoa nchini” alisema Mkuu wa Mkoa.

 

Sambamba na hilo Mhe. Batilda Burian ameweka wazi mmoja ya mkakati utakaotumika katika kupambana na ugojwa huu ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa huu wa Kipindupindu,  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu inawafikia wananchi wote.

 “Hatuna budi kuwaelimisha Wananchi na kuchukua tahadhari mapema ya kujikinga na ugonjwa huu hatari unaoambukiza kwa haraka sana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kula chakula au kunywa maji na vinywaji vingine kama juisi n.k. vilivyochafuliwa na vimelea vya Kipindupindu” aliongeza Mhe. Batilda Burin.

 

Mbali na kutoa elimu kwa Umma, Mkoa tayari umeshaandaa mpango maalumu wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu kwa kuwahusisha watalaamu wa Afya ambao watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu.

Ameleeza kuwa “Tumeandaa mpango mkakati wa Mkoa (Regional Cholera outbreak Contigency plan) wa kukabiliana na Mlipuko wa Kipindupindu endapo utatokea katika Mkoa wetu. Mpango umeianisha maeneo ya kujengea uwezo kwa wakati huu wa kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu na hatua za kuchukua endapo ugonjwa utaingia mkoani kwetu.” 

 

Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa ameendelea kumshukuru Mhe. Dkt. Sambia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha ambazo zimehimarisha kikamilifu miundombinu ya afya ambayo kwa hakika imerahisha utoaji wa huduma ya Afya na hasa sasa kwenye uwekaji wa mipango ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

 “Kwa kipekee natoa shukrani za dhati kwa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapinduzi makubwa aliyoyafanya kwenye Sekta ya Afya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wake” alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.

Mpaka sasa Mkuu wa Mkoa ameagiza Uongozi wa Halmashauri uvifahamishe  vituo vyote vya kutolea huduma za Afya kuchukua tahadhari na kutoa Elimu ya Afya kwa wagonjwa na ndugu  wa wagonjwa kujikinga na ugonjwa huu , Halmashauri zote ziandae vituo maalum tengefu (cholera Treatment Centre) watakapohudumia wagonjwa wenye Kipindupindu ,Halmashauri ziandae Mpango kazi wa kupambana na kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu kwa kushirikisha sekta muhimu za Afya, Maji na Elimu, na Maafisa Afya kusimamia na kufanya ukaguzi wa huduma na biashara za chakula, wahakikishe zinatolewa kwa kufuata kanuni na sheria za Afya 

 

 

 

 

 

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • WIZARA YA AFYA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA YAENDESHA KIKAO ELEKEZI CHA MREJESHO WA MAFUNZO NA MAPITIO YA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

    May 14, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa