Baadhi ya viongozi wa Wajasiriamali na Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi la Wanawake Mkoani Tabora wamefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian vyeti viwili vya Ushiriki kutoka SIDO na TANTRADE. Ambapo kwenye maonesho hayo Mkoa wa Tabora ulipata ushindi kwa kupeleka idadi kubwa ya wajasiriamali jumla ya 84, pamoja na bidhaa tani 11 (Asali ya Tabora ikiwemo), na kufanikiwa kuuza tani zipatazo 9.
Wakimkabidhi vyeti hivyo, viongozi hao wamemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na watendaji wake wa ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na kufanikiwa kushiriki maonesho ya Sabasaba kwa idadi kubwa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tabora amemshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha miundombinu ya barabara na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu pamoja na kutenga fedha za kuwawezesha wanawake na vijana kupitia vikundi vya ujasiriamali. Pia amewapongeza wajasiriamali Mkoani Tabora kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kwenye maonyesho hayo ambayo kwa hakika yameitangaza Mkoa wa Tabora.
Kupitia maonesho ya Sabasaba wajasiriamali kutoka Tabora wamepanua wigo wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa Mkoani Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa