• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TABORA YAPATA BILIONI 8.6 ZA RUKUZU YA MBOLEA

Posted on: October 8th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutenga fedha zaidi ya Bilioni 8.6 , kwa ajili ya ruzuku ya mbolea ambayo itakwenda kufaidisha wakulima zaidi ya elfu 29 Mkoani Tabora. Ameyasema hayo leo Oktoba, 8, 2023 alipofanya mkutano na waandishi wa Habari Ofisini kwake.

 

Mhe. Batilda Burian ameeleza kuwa, kupitia utolewaji wa fedha bilioni 8.6, Mkoa ulifanikia kupata Mbolea za aina mbalimbali tani elfu 8.2 ambayo tayari zimeshaanzwa kuwafikia wakulima elfu 29.5.

 

“Mkoa wa Tabora kupitia ruzuku hiyo ilitumia tani elfu 8.2 za mbolea mbalimbali zenye ruzuku ya Serikali bilioni 8.5 ambapo jumla ya wakulima 29,517 walinufaika na mbolea hiyo.” Alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.

 

Katika kuhakikisha wakulima wanafaidika na mbolea za ruzuku, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakulima wote Mkoani Tabora kwenda kujisajili kwenye mfumo maalumu uliowekwa na Serikali ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbolea hiyo ambayo Serikali imewekeza fedha nyingi.

 

“Niwaombe wakulima wa Mkoa wa Tabora kwenda kwenye Ofisi za Vijiji na Mitaa wakiwa na Vitambulisho vya Taifa (NIDA) au Mpiga Kura kwa ajili ya kujiandikisha kwenye vitabu vya usajili na wale waliojiandikisha mwaka jana kuhuisha taarifa zao ili waweze kunufaika na mpango wa mbolea ya ruzuku” Alisisitiza Mhe. Batilda.

 

Sambamba na hilo Mhe. Dkt Batilda Burian ametoa wito kwa wakulima wote Mkoani Tabora pamoja na mikoa ya jirani kujitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani yatakayofanyika Mkoani Tabora, na kwamba maadhimisho hayo yanalenga kuwanufaisha wakulima wote hasa upande wa teknolojia na elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea.

 

“nitumie fursa hii kuwaalika na kuwakaribisha wakulima na wadau wa sekta ya kilimo kuja kujifunza teknologia mbalimbali za matumizi sahihi ya mbolea, afya ya udongo, viuatilifu na mbegu bora ili wakulima waweze kuzalisha tija” 

 

Maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani, kwa ngazi ya Taifa yatafanyikia Mkoani Tabora kwenye viwanja vya Chipukizi, Manispaa ya Tabora kuanzia Oktoba 11, 2023 hadi Oktoba 13, 2023. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Matumizi Sahihi ya Mbolea ya Ruzuku kwa Kilimo chenye Tija”. 

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa