Leo Julai 26, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amewapokea wageni kumi (10) kutoka Afrika Kusini ambao wamekuja Mkoani Tabora kwa Lengo la kujifunza masuala ya Ufugaji Nyuki. Ugeni huu utakuwa na ziara ya siku tatu (3).
Ikubukwe, Mkoa wa Tabora ulishiriki Kongamano la ufugaji nyuki la APIMONDIA la Bara la Afrika lililofanyika Durban nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 21-24 Machi, 2023 ambalo lilikutanisha wadau wa asali kutoka duniani kote. Mkoa wa Tabora ulifanikiwa kutuma wajumbe wake ambao walifanikiwa kuitambulisha asali ya Tabora katika viwango vya ubora vya kimataifa na kupatiwa cheti.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa