TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora imefanikiwa kuokoa na kurejesha kiasi cha shilingi milioni 794.1 katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Taboea Mashauri Elisante alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu kwa waandishi wa habari.
Alisema kati ya fedha hizo shilingi milioni 339.4 ziliokolewa kutokana na michango ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSSF) ya wafanyakazi ambayo haikuwasilishwa na Kampuni ya JIANGXI CEO Engineering, milioni 271 zilirejeshwa mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,(PSSF) kutoka Tabora Railways Saccos ambazo walikuwa wamekopeshwa tangu 2015 na milioni 136.8 zilirejeshwa Tabora Railway Saccos kutoka Railway Corporation Makao Makuu.
Elisante alitaja fedha nyingine kuwa ni shilingi milioni 8.8 ambazo zilirejeshwa katika vyama vya ushirika (AMCOS) , milioni 19.9 ziliokolewa kutokana na mikopo humiza na kurejeshwa kwa watumishi wastaafu na kiasi cha milioni 15 zilireshwa na Mtumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) baada ya kumkamata pasipo kufuata taratibu mfanyabiashara wakati wa zoezi la ukaguzi.
Katika hatua nyingine Elisante alisema TAKUKURU Mkoa wa Tabora katika kipindi cha miezi mitatu imepokea jumla ya malalamiko 116 ambapo kati yake 50 yalikuwa na viashiri vya rushwa na 66 hayakuwa na viashiri vya rushwa.
Aliongeza kuwa kati ya malalamiko hayo 8 yalihamishiwa kwenye Idara zingine kwa ufuatuliaji na majalada 7 yamekamilika na wamefungua kesi tano mpya.
Aidha Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora alitoa wito kwa wananchui kuendelea kuunga mkono juhudi za TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa kupitia namba husika.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa