Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Matiko Chacha, amefanya ziara ya ukaguziwa miradi ya maendeleo katika wilaya za Uyui, Urambo na Kaliua. Ziara hiyo ikilengakusimamia utendaji serikalini na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama ChaMapinduzi (CCM).
Mhe. Chacha amekagua mradi wa ujenzi wa jengo laupasuaji na jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya Hassan Wakasuvikilichopo Kata ya Mabama, Wilaya ya Uyui. Mradi huo unagharimu shilingi milioni232, na umefikia asilimia 85 ya utekelezaji.
Aidha, Mhe. Chacha alikagua ujenzi wa Kituo chaAfya Vumilia kilichopo Wilaya ya Urambo, ambapo ujenzi umekamilika kwa asilimia100. Serikali tayari imetoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba, ambapo vifaa vya awamu ya kwanza vyenye thamani ya shilingi milioni 250tayari vimekwisha pokelewa, Vilevile Ujenzi wa Kituo cha Afya Songambele piaumekamilika kwa asilimia 100.
Hata hivyo, Mhe. Chacha hakuridhishwa na ujenziwa Kituo cha Afya Igagala kilichopo Wilaya ya Kaliua. Ametoa maelekezo kwa Mkuuwa Wilaya ya Kaliua, Mhe.Dkt. Gerald Mongela, kuhakikisha ujenzi wa kichomeataka unakamilika kwa wakati ili kituo hicho kiweze kutoa huduma kwa ukamilifu.
Akizungumza na wananchi wa Uyui na Urambo,Mhe. Chacha aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya hospitali ili iwezekudumu na kutoa huduma bora. Alisisitiza kuwa miundombinu hiyo inajengwa kwaajili ya wananchi na kuwataka kuwa walinzi wa vifaa vinavyotolewa na serikali.Aliwahimiza pia wananchi kuacha imani za kishirikina na kutumia huduma zahospitali badala ya kutafuta waganga wa kienyeji pindi wanapopata changamoto zakiafya.
Wananchi wa Wilaya yaUrambo na Uyui wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi zamaendeleo, hasa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati. Wameahidikuendelea kumuombea Rais pamoja na viongozi wote ili waendelee kutekeleza majukumuyao kwa ufanisi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa