Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt.John Mboya amewataka wanawake wa UWT Mkoani Tabora kutumia muda wao kuelezea kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kwani tangu aingie madarakani Mkoa wa Tabora umepokea fedha nyingi ambazo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo. Ameyasema hayo leo Julai, 7 2023 alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwenye uzinduzi wa miradi kwa kata 206 ya wanawake Mkoani Tabora inayotolewa na Mhe. Jaqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoani.
Dkt.John Mboya ameeleza kuwa, “kumefanyika maboresho makubwa sana katika sekta ya afya, miundombinu ya barabara na sasa ujenzi wa reli ya kisasa na ukamilishwaji wa miradi ya elimu kupitia program ya BOOST. Na hivyo kuna kila sababu ya kuwaelezea watanzania kazi zinazofanywa na Serikali yetu.”
Aidha Dkt. Mboya amempongeza Mhe Jaqueline Kainja kwa kutoa fedha Tsh. Milioni Themanini na moja(81,000,000) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya wanawake ambayo kwa hakika inakwenda kuwasaidia wanawake wengi. “Na sisi kama serikali tutahakikisha tunatumia wadau wetu katika kusimamia miradi mbalimbali inayowahusu wanawake na nitoe wito kwenu kuwa fedha hizi mzitumie kwa malengo yaliowekwa” alisema
Na kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Dkt. John Mboya alimkabidhi jumla ya Shilingi Milioni Themanini na moja (81,000,000) Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Ndugu, Mwanne Mchemba kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya wanawake Mkoani Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa