Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian leo Julai 14, 2023, ameanza ziara yake Wilayani Igunga kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo (Elimu na Afya) ikiwemo ile miradi ya ujenzi wa shule mpya kupitia Program ya BOOST. Ambapo ameanza ziara yake kwa kufanya ukaguzi kwenye ujenzi wa shule mpya ya Msingi Jitegemee.l na Matinje.
Ikumbukwe kuwa, Kupitia Program ya BOOST, Mkoa wa Tabora umepata jumla ya shilingi Bilioni 12.1 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi mpya 17, vyumba vya madarasa 118, vyumba vya madarasa ya mfano ya Elimu ya Awali 16, matundu ya vyoo 130 na nyumba za walimu 2 (2 in 1). Ambapo wilaya ya Igunga ilipata jumla ya shilingi Bilioni 1.3 ambapo shule mbili (2) mpya za msingi zinaendelea kujengwa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa